1 Kings 22:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Mikaya akasema, “Haya sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Nilimwona Mwenyezi-Mungu ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni limesimama kando yake, upande wake wa kulia na wa kushoto;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la Mwenyezi Mungu: Nilimwona Mwenyezi Mungu ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Mikaya akasema, “Haya sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Nilimwona Mwenyezi-Mungu ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni limesimama kando yake, upande wake wa kulia na wa kushoto;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la BWANA: Nilimwona BWANA ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni wamesimama kumzunguka kulia kwake na kushoto kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mikaya akaendelea, “Kwa hiyo lisikie neno la bwana: Nilimwona bwana ameketi juu ya kiti chake cha enzi pamoja na jeshi lote la mbinguni likiwa limesimama kumzunguka upande wa kulia na wa kushoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Mikaya akasema, “Haya sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Nilimwona Mwenyezi-Mungu ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni limesimama kando yake, upande wake wa kulia na wa kushoto;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mikaya akasema: Lakini lisikie neno la Bwana! Nimemwona Bwana, akikaa katika kiti chake kitukufu, navyo vikosi vyote vya mbinguni vilisimama mbele yake, kuumeni na kushotoni kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nalimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Mikaya akasema: “Sasa sikia neno la Yawe: Nilimwona Yawe akiikaa katika kiti chake cha kifalme, na jeshi lote la mbinguni likisimama pembeni yake, upande wake wa kuume na wa kushoto.