1 Kings 22:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru makapteni wake thelathini na wawili waliosimamia magari yake ya kukokotwa, akisema: “Msipigane na mtu yeyote yule, mkubwa au mdogo, ila tu na mfalme wa Israeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru wakuu wa magari yake thelathini na wawili, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru makapteni wake thelathini na wawili waliosimamia magari yake ya kukokotwa, akisema: “Msipigane na mtu yeyote yule, mkubwa au mdogo, ila tu na mfalme wa Israeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na ye yote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huu, mfalme wa Aramu alikuwa amewaagiza majemadari thelathini na wawili wa magari ya vita, “Msipigane na yeyote, mdogo au mkubwa, isipokuwa mfalme wa Israeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru wakuu wa magari yake thelathini na wawili, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru makapteni wake thelathini na wawili waliosimamia magari yake ya kukokotwa, akisema: “Msipigane na mtu yeyote yule, mkubwa au mdogo, ila tu na mfalme wa Israeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mfalme wa Ushami alikuwa amewaagiza wakuu wake wa magari 32 kwamba: Msipigane na mtu ye yote, mdogo kwa mkubwa, ila mpigane na mfalme wa Waisiraeli peke yake tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru wakuu wa magari yake thelathini na wawili, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme wa Aramu alikuwa amewaamuru viongozi wake makumi tatu na wawili waliosimamia magari yake ya vita, akisema: “Musishambulie mutu yeyote, mukubwa au mudogo, lakini tu mufalme wa Israeli.”