1 Kings 22:38 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gari lake la kukokotwa waliliosha katika bwawa la Samaria, mbwa wakairamba damu yake, nao makahaba wakaoga humo, sawa kabisa na neno alilosema Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakaramba damu yake, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu lilivyokuwa limesema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la Bwana alilolinena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gari lake la kukokotwa waliliosha katika bwawa la Samaria, mbwa wakairamba damu yake, nao makahaba wakaoga humo, sawa kabisa na neno alilosema Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakalamba damu yake, sawasawa na neno la BWANA lilivyokuwa limesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakasafisha lile gari la vita katika bwawa la Samaria (mahali makahaba walipooga), na mbwa wakaramba damu yake, sawasawa na neno la bwana lilivyokuwa limesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la BWANA alilolinena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gari lake la kukokotwa waliliosha katika bwawa la Samaria, mbwa wakairamba damu yake, nao makahaba wakaoga humo, sawa kabisa na neno alilosema Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipolisafisha lile gari kwa maji penye ziwa la Samaria, mbwa wakailamba damu yake nao wanawake wagoni wakaoga papo hapo, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la BWANA alilolinena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gari lake la vita walilisafisha katika kisima cha Samaria, imbwa wakailamba damu yake, nao makahaba wakaoga mule, sawa kabisa na neno Yawe alilosema.