1 Kings 22:50 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hatimaye, Yehoshafati alifariki, na kuzikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi baba yake; naye Yehoramu, mwanawe, akatawala mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Yehoramu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake; na Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Ahazia mwana wa Ahabu, akamwambia Yehoshafati, “Waache watumishi wangu wasafiri pamoja na watumishi wako katika meli.” Lakini Yehoshafati hakukubali jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yehoshafati akalala na baba zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Naye Yehoramu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake; na Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hatimaye, Yehoshafati alifariki, na kuzikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi baba yake; naye Yehoramu, mwanawe, akatawala mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile Ahazia, mwana wa Ahabu, alimwambia Yosafati: Watumishi wangu, na waende pamoja na watumishi wako merikebuni. Lakini Yosafati akakataa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake; na Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yosafati: “Uwaache watumishi wangu wasafiri pamoja na watumishi wako katika mashua.” Lakini Yosafati hakukubali jambo hilo.