1 Kings 22:51 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Ahazia, mwana wa Ahabu, alianza kutawala Israeli. Alitawala kwa muda wa miaka miwili, kutoka Samaria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Naye akatawala katika Israeli kwa miaka miwili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria, katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka miwili juu ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hatimaye, Yehoshafati alifariki, na kuzikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi baba yake; naye Yehoramu, mwanawe, akatawala mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye alitawala katika Israeli kwa miaka miwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye alitawala katika Israeli kwa miaka miwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria, katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka miwili juu ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Ahazia, mwana wa Ahabu, alianza kutawala Israeli. Alitawala kwa muda wa miaka miwili, kutoka Samaria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosafati akaja kulala na baba zake, akazikwa kwa baba zake mjini mwa baba yake Dawidi, naye mwanawe Yoramu akawa mfalme mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria, katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka miwili juu ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mwisho, Yosafati akakufa, akazikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika muji wa Daudi babu yake. Naye Yoramu mwana wake akatawala kwa pahali pake.