1 Kings 22:52 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ahazia alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; aliuiga mwenendo wa baba yake na mwenendo wa Yezebeli, mama yake, na wa Yeroboamu, mwana wa Nebati ambaye aliwafanya watu wa Israeli watende dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Ahazia, mwana wa Ahabu, alianza kutawala Israeli. Alitawala kwa muda wa miaka miwili, kutoka Samaria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akafanya maovu machoni mwa BWANA kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafanya maovu machoni mwa bwana kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ahazia alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; aliuiga mwenendo wa baba yake na mwenendo wa Yezebeli, mama yake, na wa Yeroboamu, mwana wa Nebati ambaye aliwafanya watu wa Israeli watende dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahazia, mwana wa Ahabu, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli kule Samaria katika mwaka wa 17 wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, akawa mfalme wa Waisiraeli miaka 2.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Yosafati mufalme wa Yuda, Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala Israeli. Alitawala kwa muda wa miaka miwili, akiwa Samaria.