1 Kings 3:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alipoamka, alitambua kwamba ilikuwa ndoto. Ndipo akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, akamtolea tambiko za kuteketezwa na za amani. Halafu akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Sulemani akaamka, akatambua kuwa ilikuwa ndoto. Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Bwana, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alipoamka, alitambua kwamba ilikuwa ndoto. Ndipo akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, akamtolea tambiko za kuteketezwa na za amani. Halafu akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Solomoni akaamka, akatambua kuwa alikuwa katika ndoto. Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la BWANA, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Sulemani akaamka, akatambua kuwa ilikuwa ndoto. Akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la bwana, naye akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha akawafanyia watumishi wake wote karamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la Agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alipoamka, alitambua kwamba ilikuwa ndoto. Ndipo akarudi Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, akamtolea tambiko za kuteketezwa na za amani. Halafu akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo alipoamka akaona, ya kuwa ameota; alipofika Yerusalemu, akaja kusimama mbele ya Sanduku la Agano la Bwana, akatoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, akatengeneza nazo ng'ombe za tambiko za shukrani, akawafanyia watumishi wake wote karamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alipoamuka, alitambua kwamba ilikuwa ndoto. Halafu akarudi Yerusalema, akasimama mbele ya Sanduku la Agano la Yawe, akamutolea sadaka za kuteketezwa na za amani. Halafu akawafanyia watumishi wake wote karamu.