1 Kings 3:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilipoamka asubuhi na kutaka kumnyonyesha mwanangu, nikakuta mtoto amefariki. Nilipochunguza sana, nikagundua kuwa hakuwa mwanangu niliyemzaa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia kwa makini katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyemzaa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilipoamka asubuhi na kutaka kumnyonyesha mwanangu, nikakuta mtoto amefariki. Nilipochunguza sana, nikagundua kuwa hakuwa mwanangu niliyemzaa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asubuhi yake, nikaamka ili kumnyonyesha mwanangu, naye alikuwa amekufa! Lakini nilipomwangalia sana katika nuru ya asubuhi, niliona kuwa hakuwa yule mwana niliyekuwa nimemzaa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilipoamka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe. Amekufa. Na asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilipoamka asubuhi na kutaka kumnyonyesha mwanangu, nikakuta mtoto amefariki. Nilipochunguza sana, nikagundua kuwa hakuwa mwanangu niliyemzaa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asubuhi nilipoamka kumnyonyesha mtoto wangu, nikimtazama, amekufa. Kulipokucha vema, nikamchungulia sana, nimtambue, nikamwona, ya kuwa si mtoto wangu, niliyemzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilipoamuka asubui na kutaka kumunyonyesha mwana wangu, nikakuta mutoto amekufa. Nilipochunguza sana, nikagundua kwamba hakukuwa mwana wangu niliyemuzaa.”