1 Kings 3:28 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wa Israeli waliposikia juu ya hukumu ya mfalme, walimwogopa, wakatambua kwamba alikuwa na hekima ya Mungu iliyomwezesha kutoa hukumu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wa Israeli waliposikia juu ya hukumu ya mfalme, walimwogopa, wakatambua kwamba alikuwa na hekima ya Mungu iliyomwezesha kutoa hukumu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Israeli yote iliposikia hukumu aliyotoa mfalme, wakamwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa alikuwa na hekima kutoka kwa Mungu kwa kutoa haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wa Israeli waliposikia juu ya hukumu ya mfalme, walimwogopa, wakatambua kwamba alikuwa na hekima ya Mungu iliyomwezesha kutoa hukumu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waisiraeli wote wakasikia, mfalme alivyolikata lile shauri, wakamwogopa mfalme, kwani wameona, ya kuwa moyoni mwake umo werevu wa Kimungu wa kuwaamulia watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wa Israeli waliposikia juu ya hukumu ya mufalme, walimwogopa. Wakatambua kwamba alikuwa na hekima ya Mungu iliyomuwezesha kutoa hukumu za haki.