1 Kings 3:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mmoja, Solomoni alikwenda kutoa tambiko huko Gibeoni, maana palikuwa ndipo mahali maarufu pa ibada. Ilikuwa ni kawaida ya Solomoni kutoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa katika madhabahu hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali pa juu pa kuabudia pakuu, naye Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hayo madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mmoja, Solomoni alikwenda kutoa tambiko huko Gibeoni, maana palikuwa ndipo mahali maarufu pa ibada. Ilikuwa ni kawaida ya Solomoni kutoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa katika madhabahu hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali maarufu zaidi, naye Solomoni akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hiyo madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akaenda Gibeoni kutoa dhabihu, kwa maana ndipo palipokuwa mahali pa juu pa kuabudia, naye Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya hayo madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mmoja, Solomoni alikwenda kutoa tambiko huko Gibeoni, maana palikuwa ndipo mahali maarufu pa ibada. Ilikuwa ni kawaida ya Solomoni kutoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa katika madhabahu hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akaenda Gibeoni kutambika huko, kwani hicho kilikuwa kilima kikuu cha kutambikia juu yake; Salomo akatoa ng'ombe elfu za tambiko za kuteketezwa nzima hapo pa kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati mumoja, Solomono alikwenda kutoa sadaka kule kwenye kilima cha Gibeoni, maana palikuwa ndipo pahali pakubwa pa ibada. Ilikuwa ni kawaida ya Solomono kutoa maelfu ya sadaka za kuteketezwa katika mazabahu hiyo.