1 Kings 3:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umeniweka mimi mtumishi wako kuwa mfalme mahali pa baba yangu Daudi, ijapokuwa ningali mtoto mdogo na sijui namna ya kutekeleza wajibu huu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme mahali pa baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu, wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umeniweka mimi mtumishi wako kuwa mfalme mahali pa baba yangu Daudi, ijapokuwa ningali mtoto mdogo na sijui namna ya kutekeleza wajibu huu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa, Ee BWANA Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme baada ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa, Ee bwana Mwenyezi Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako mfalme badala ya baba yangu Daudi. Lakini mimi ni mtoto mdogo tu, wala sijui jinsi ya kutekeleza wajibu wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umeniweka mimi mtumishi wako kuwa mfalme mahali pa baba yangu Daudi, ijapokuwa ningali mtoto mdogo na sijui namna ya kutekeleza wajibu huu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa Bwana Mungu wangu, wewe umempa mtumishi wako kuwa mfalme mahali pa baba yangu Dawidi, nami nikingali mwana mdogo bado, sijui penye kutoka wala penye kuingia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, Mungu wangu, umeniweka mimi mutumishi wako kuwa mufalme pahali pa baba yangu Daudi, ijapokuwa ningali mutoto mudogo na sijui namna ya kutimiza kazi hii.