1 Kings 4:21 — Compare Translations

10 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alitawala falme zote kuanzia mto Eufrate mpaka nchi ya Wafilisti, hadi mpakani na Misri. Mataifa yote yalimtumikia na kulipa kodi kwake wakati wote wa maisha yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Sulemani akatawala katika falme zote kuanzia Mto hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Sulemani, siku zote za maisha yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alitawala falme zote kuanzia mto Eufrate mpaka nchi ya Wafilisti, hadi mpakani na Misri. Mataifa yote yalimtumikia na kulipa kodi kwake wakati wote wa maisha yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Solomoni akatawala katika falme zote kuanzia Mto Eufrati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Solomoni, siku zote za maisha yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Sulemani akatawala katika falme zote kuanzia Mto Frati hadi nchi ya Wafilisti, hadi kwenye mpaka wa Misri. Nchi hizi zilileta ushuru na zilikuwa chini ya Sulemani, siku zote za maisha yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alitawala falme zote kuanzia mto Eufrate mpaka nchi ya Wafilisti, hadi mpakani na Misri. Mataifa yote yalimtumikia na kulipa kodi kwake wakati wote wa maisha yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akawa akizitawala nchi za kifalme zote kutoka lile jito kubwa kuifikia nchi ya Wafilisti hata mipaka ya Misri; walimletea mahongo, wakamtumikia Salomo siku zake zote za kuwapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.