1 Kings 4:27 — Compare Translations
10 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale maofisa wake kumi na wawili, kila mmoja kwa mwezi aliopangiwa, walipeleka chakula cha kutosha kwa ajili ya mfalme na wale wote waliokula nyumbani mwake. Mahitaji yao yote yalitoshelezwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Sulemani na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na maakida wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale maofisa wake kumi na wawili, kila mmoja kwa mwezi aliopangiwa, walipeleka chakula cha kutosha kwa ajili ya mfalme na wale wote waliokula nyumbani mwake. Mahitaji yao yote yalitoshelezwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Solomoni na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna cho chote kilichopungua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wa eneo hilo, kila mmoja katika mwezi wake, walileta mahitaji kwa ajili ya Mfalme Sulemani na wote waliokula mezani mwa mfalme. Walihakikisha kuwa hakuna chochote kilichopungua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na maofisa wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale maofisa wake kumi na wawili, kila mmoja kwa mwezi aliopangiwa, walipeleka chakula cha kutosha kwa ajili ya mfalme na wale wote waliokula nyumbani mwake. Mahitaji yao yote yalitoshelezwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wale waangaliaji wakampatia mfalme Salomo vyakula nao wote walioikaribia meza ya mfalme Salomo, kila mmoja wao mwezi wake, hawakuwakosesha kitu cho chote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)