1 Kings 4:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni aliteua maofisa tawala kumi na wawili kwa nchi nzima ya Israeli. Hao walipewa jukumu la kutafuta chakula kwa ajili ya mfalme na nyumba yake; kila mmoja wao alileta chakula kutoka mkoani kwake kwa mwezi mmoja kila mwaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Sulemani alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioshughulikia mahitaji ya mfalme na ya watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni aliteua maofisa tawala kumi na wawili kwa nchi nzima ya Israeli. Hao walipewa jukumu la kutafuta chakula kwa ajili ya mfalme na nyumba yake; kila mmoja wao alileta chakula kutoka mkoani kwake kwa mwezi mmoja kila mwaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Solomoni alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Sulemani alikuwa na watawala kumi na wawili wa wilaya katika Israeli yote, walioleta mahitaji kwa mfalme na kwa watu wa nyumbani kwa mfalme. Kila mmoja alitoa chakula kwa mwezi mmoja katika mwaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani alikuwa na maafisa tawala kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni aliteua maofisa tawala kumi na wawili kwa nchi nzima ya Israeli. Hao walipewa jukumu la kutafuta chakula kwa ajili ya mfalme na nyumba yake; kila mmoja wao alileta chakula kutoka mkoani kwake kwa mwezi mmoja kila mwaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo alikuwa na waangaliaji kumi na wawili waliowekwa kuwaangalia Waisiraeli wote, ndio waliompatia mfalme nao wa nyumbani mwake vyakula, ikawa kila mmoja akaleta vyakula vya mwezi mmoja katika mwaka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alichagua maliwali kumi na wawili kwa inchi nzima ya Israeli. Hao walipewa kazi ya kutafuta chakula kwa ajili ya mufalme na nyumba yake. Kila mumoja wao alileta chakula kutoka jimbo lake kwa mwezi mumoja kila mwaka.