1 Kings 5:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu akampa Solomoni hekima kama alivyomwahidi. Kukawa na amani kati ya Solomoni na Hiramu; wakafanya mkataba kati yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwa na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Sulemani, na wote wawili wakafanya mkataba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanyana maagano pamoja hao wawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu akampa Solomoni hekima kama alivyomwahidi. Kukawa na amani kati ya Solomoni na Hiramu; wakafanya mkataba kati yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akampa Solomoni hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Solomoni, na wote wawili wakafanya mkataba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwepo na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Sulemani, na wote wawili wakafanya mkataba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanya mikataba kati yao wawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu akampa Solomoni hekima kama alivyomwahidi. Kukawa na amani kati ya Solomoni na Hiramu; wakafanya mkataba kati yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akampa Salomo werevu wa kweli, kama alivyomwambia. Kwao Hiramu na Salomo yakawako matengemano, wakafanya agano hao wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidia. Ikawa amani kati yao Hiramu na Sulemani; wakafanyana maagano pamoja hao wawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitunga mezali elfu tatu na nyimbo elfu moja na tano.