1 Kings 5:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wajua kwamba baba yangu Daudi hakuweza kumjengea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, hekalu la kumwabudia, kwa sababu ya kukumbana na vita vingi dhidi ya maadui wa nchi jirani mpaka hapo Mwenyezi-Mungu alipompatia ushindi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Unajua kwamba baba yangu Daudi hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi yake kutoka pande zote, hadi Mwenyezi Mungu alipowaweka adui zake chini ya miguu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umemjua Daudi baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata Bwana alipowatia watu chini ya nyayo zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wajua kwamba baba yangu Daudi hakuweza kumjengea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, hekalu la kumwabudia, kwa sababu ya kukumbana na vita vingi dhidi ya maadui wa nchi jirani mpaka hapo Mwenyezi-Mungu alipompatia ushindi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la BWANA Mungu wake, hadi BWANA alipowaweka adui zake chini ya miguu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Unajua kwamba kwa sababu ya vita vilivyopiganwa dhidi ya baba yangu Daudi kutoka pande zote, hakuweza kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la bwana Mwenyezi Mungu wake, hadi bwana alipowaweka adui zake chini ya miguu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wajua kuwa Daudi baba yangu hakuweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wajua kwamba baba yangu Daudi hakuweza kumjengea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, hekalu la kumwabudia, kwa sababu ya kukumbana na vita vingi dhidi ya maadui wa nchi jirani mpaka hapo Mwenyezi-Mungu alipompatia ushindi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wewe unajua, ya kuwa baba yangu Dawidi hakuweza kulijengea Jina la Bwana Mungu wake nyumba kwa ajili ya vita, adui zake walivyomletea toka pande zote, hata Bwana akawaweka chini ya nyayo za miguu yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umemjua Daudi baba yangu jinsi asivyoweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
ngombe wanono kumi, na ngombe makumi mbili toka shamba la malisho, kondoo mia moja pamoja na kulungu, paa, swala na kuku wanono.