1 Kings 5:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hiramu alifurahi sana alipopata ujumbe huu wa Solomoni, akasema, “Mwenyezi-Mungu asifiwe wakati huu, kwa kumpa Daudi mwana mwenye hekima atawale taifa hili kubwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hiramu aliposikia ujumbe wa Sulemani, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima ya kutawala taifa hili kubwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe Bwana leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hiramu alifurahi sana alipopata ujumbe huu wa Solomoni, akasema, “Mwenyezi-Mungu asifiwe wakati huu, kwa kumpa Daudi mwana mwenye hekima atawale taifa hili kubwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hiramu aliposikia ujumbe wa Solomoni, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe BWANA leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima kutawala juu ya taifa hili kubwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hiramu aliposikia ujumbe wa Sulemani, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe bwana leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima kutawala juu ya taifa hili kubwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe BWANA leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hiramu alifurahi sana alipopata ujumbe huu wa Solomoni, akasema, “Mwenyezi-Mungu asifiwe wakati huu, kwa kumpa Daudi mwana mwenye hekima atawale taifa hili kubwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Hiramu alipoyasikia haya maneno ya Salomo akafurahi sana, akasema: Bwana na atukuzwe leo hivi, kwani amempa Dawidi mwana mwenye werevu wa kweli wa kuwatawala wale watu wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe BWANA leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale maliwali wake kumi na wawili, kila mumoja kwa mwezi aliopangiwa, walipeleka chakula cha kutosha kwa ajili ya mufalme na wale wote waliokula katika nyumba yake. Mahitaji yao yote yalitoshelezwa.