1 Kings 5:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Hiramu alimpelekea Solomoni ujumbe, akisema, “Nimepokea ujumbe wako, nami niko tayari kutimiza mahitaji yako kuhusu mbao za mierezi na za miberoshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Hiramu akapeleka ujumbe kwa Sulemani: “Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mwerezi na misunobari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeyasikia yale uliyoniletea; nami nitafanya kila ulitakalo katika habari ya miti ya mierezi, na miti ya miberoshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Hiramu alimpelekea Solomoni ujumbe, akisema, “Nimepokea ujumbe wako, nami niko tayari kutimiza mahitaji yako kuhusu mbao za mierezi na za miberoshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hiramu akatuma neno kwa Solomoni: “Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mierezi na misunobari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hiramu akatuma neno kwa Sulemani: “Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mierezi na misunobari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeusikia ujumbe ulionitumia; nami nitafanya kila ulitakalo kuhusu miti ya mierezi, na miti ya miberoshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Hiramu alimpelekea Solomoni ujumbe, akisema, “Nimepokea ujumbe wako, nami niko tayari kutimiza mahitaji yako kuhusu mbao za mierezi na za miberoshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Hiramu alipotuma kwa Salomo kumwambia: Nimeyasikia maneno yako, uliyotuma kuniambia. Mimi nitayafanya yote, uyatakayo, nikupatie miti ya miangati na miti ya mivinje.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeyasikia yale uliyoniletea; nami nitafanya kila ulitakalo katika habari ya miti ya mierezi, na miti ya miberoshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zamu ya kila mumoja ilipofika, alipeleka vilevile shayiri na majani ya kulisha farasi na nyama wanaokimbia mbio.