1 Kings 6:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka Misri. Huo ulikuwa mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni juu ya Israeli, katika mwezi wa Zifu, yaani mwezi wa pili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, uliokuwa mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka Misri. Huo ulikuwa mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni juu ya Israeli, katika mwezi wa Zifu, yaani mwezi wa pili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya wana wa Israeli kutoka nchini Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alianza kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka Misri. Huo ulikuwa mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni juu ya Israeli, katika mwezi wa Zifu, yaani mwezi wa pili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa katika mwaka wa 480, tangu wana wa Isiraeli walipotoka Misri, katika mwaka wa nne, Salomo alipokuwa mfalme wa Waisiraeli, katika mwezi wa Ziwu, ndio mwezi wa pili, ndipo, alipomjengea Bwana nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa katika mwaka wa mia nne na themanini baada ya kutoka wana wa Israeli katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa kutawala kwake Sulemani juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa pili, akaanza kuijenga nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alianza kujenga nyumba ya Yawe katika mwaka wa mia ine na makumi nane kisha Waisraeli kutoka Misri. Huo ulikuwa mwaka wa ine wa utawala wa Solomono juu ya Israeli, katika mwezi wa Zivu, ni kusema mwezi wa pili.