1 Kings 6:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chumba cha ndani, kilichoitwa mahali patakatifu sana, kilijengwa katika sehemu ya nyuma ya nyumba. Kilikuwa kimejengwa kwa mbao za mierezi kutoka sakafuni hadi darini, na urefu wake ulikuwa mita 9.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mwerezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chumba cha ndani, kilichoitwa mahali patakatifu sana, kilijengwa katika sehemu ya nyuma ya nyumba. Kilikuwa kimejengwa kwa mbao za mierezi kutoka sakafuni hadi darini, na urefu wake ulikuwa mita 9.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu ya ndani ya patakatifu, yaani Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chumba cha ndani, kilichoitwa mahali patakatifu sana, kilijengwa katika sehemu ya nyuma ya nyumba. Kilikuwa kimejengwa kwa mbao za mierezi kutoka sakafuni hadi darini, na urefu wake ulikuwa mita 9.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akajenga chumba mle nyumbani upande wa nyuma urefu wa mikono 20 kwa mbao za miangati kuanzia chini mpaka juu ukutani; ndivyo, alivyojenga mle nyumbani chumba cha nyuma kuwa Patakatifu Penyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chumba cha ndani, kilichoitwa Pahali Patakatifu Sana, kilijengwa katika sehemu ya nyuma ya nyumba. Kilikuwa kimejengwa kwa mbao za mierezi kutokea kwenye sakafu mpaka kwenye dari, na urefu wake ulikuwa metre tisa.