1 Kings 6:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sanamu hizo zilikuwa sambamba, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: Bawa la mmoja likigusa ukuta mmoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, huku yale mengine yaligusana katikati ya chumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliwaweka makerubi hao katika chumba cha ndani kabisa cha Hekalu, mabawa yao yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta wa upande mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sanamu hizo zilikuwa sambamba, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: bawa la mmoja likigusa ukuta mmoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, huku yale mengine yaligusana katikati ya chumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sanamu hizo zilikuwa sambamba, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: Bawa la mmoja likigusa ukuta mmoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, huku yale mengine yaligusana katikati ya chumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akayaweka haya Makerubi katikati ya chumba cha ndani, yakiwa yameyakunjua mabawa yao, bawa la moja liligusa ukuta, nalo bawa lake lile la pili liligusa ukuta wa pili, nayo mabawa yao yaliyoelekea upande wa nyumbani kati yaligusana bawa kwa bawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani; na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko; mabawa yao yakagusana katikati ya nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sanamu hizo zilielekeana, zikiwa na mabawa yaliyokunjuliwa: bawa la mumoja likigusa ukuta mumoja, na bawa la mwingine likigusa ukuta wa pili, na yale mengine yaligusana katikati ya chumba.