1 Kings 6:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika milango hiyo miwili ya mizeituni, alichora viumbe wenye mabawa, mitende na maua yaliyochanua; akaipamba michoro hiyo kwa dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwenye milango hiyo miwili ya mbao za mzeituni, alinakshi makerubi, mitende, pamoja na maua yaliyochanua, na kufunika makerubi na mitende kwa dhahabu iliyofuliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika milango hiyo miwili ya mizeituni, alichora viumbe wenye mabawa, mitende na maua yaliyochanua; akaipamba michoro hiyo kwa dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Juu ya milango miwili ya mbao za mzeituni alinakshi makerubi, miti ya mitende pamoja na maua yaliyochanua na kufunika makerubi na miti ya mitende kwa dhahabu iliyofuliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Juu ya milango miwili ya mbao za mzeituni alinakshi makerubi, miti ya mitende pamoja na maua yaliyochanua na kufunika makerubi na miti ya mitende kwa dhahabu iliyofuliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika milango hiyo miwili ya mizeituni, alichora viumbe wenye mabawa, mitende na maua yaliyochanua; akaipamba michoro hiyo kwa dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo katika hiyo milango miwili ya mbao za michekele akachora machoro ya Makerubi na ya mitende na ya maua yachanukayo, kisha akaifunikiza dhahabu; hizo dhahabu za kuyafunikiza Makerubi na mitende zilikuwa zimesanwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo akafanya milango miwili ya mzeituni; akanakshi juu yake nakshi za makerubi, na mitende, na maua yaliyofunuka wazi, akaifunika kwa dhahabu; akatia dhahabu juu ya makerubi, na juu ya mitende.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika milango hiyo miwili ya mizeituni, alichora makerubi, miti ya ngazi na maua yaliyochanua; akaipamba michoro hiyo kwa zahabu.