1 Kings 6:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia alijenga nguzo kuzunguka, ili kutegemeza ukuta wa nje; akatengeneza na vyumba vya pembeni kila upande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akajenga vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote, vikishikamana na kuta za ukumbi wa Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao ukuta wa nyumba akauzungushia vyumba, kushikamana na kuta za nyumba kote kote, za hekalu na za chumba cha ndani; akafanya vyumba vya mbavuni pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia alijenga nguzo kuzunguka, ili kutegemeza ukuta wa nje; akatengeneza na vyumba vya pembeni kila upande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao ukuta wa nyumba akauzungushia vyumba, kushikamana na kuta za nyumba kotekote, za hekalu na za chumba cha ndani; akafanya vyumba vya mbavuni pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia alijenga nguzo kuzunguka, ili kutegemeza ukuta wa nje; akatengeneza na vyumba vya pembeni kila upande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kando ya ukuta wa nyumba kuizunguka yote akajenga vyumba vilivyozizunguka kuta za nyumba pande zote za hapo Patakatifu napo hapo penye chumba cha nyuma; hivyo vyumba akavitengeneza ubavuni pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao ukuta wa nyumba akauzungushia vyumba, kushikamana na kuta za nyumba kote kote, za hekalu na za chumba cha ndani; akafanya vyumba vya mbavuni pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena aliongeza kujenga nguzo kuzunguka, kwa kutegemeza ukuta wa inje. Akatengeneza vyumba vya pembeni kila upande.