1 Kings 7:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo, alikuwa mwana wa mjane wa kabila la Naftali, na baba yake alikuwa mkazi wa Tiro, mfua shaba. Hiramu alikuwa na hekima nyingi na akili, na fundi stadi wa kazi yoyote ya shaba. Basi, alikuja kwa mfalme Solomoni, akamfanyia kazi yake yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Sulemani na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila ya Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, mstadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikilia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo, alikuwa mwana wa mjane wa kabila la Naftali, na baba yake alikuwa mkazi wa Tiro, mfua shaba. Hiramu alikuwa na hekima nyingi na akili, na fundi stadi wa kazi yoyote ya shaba. Basi, alikuja kwa mfalme Solomoni, akamfanyia kazi yake yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Solomoni na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Sulemani na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo, alikuwa mwana wa mjane wa kabila la Naftali, na baba yake alikuwa mkazi wa Tiro, mfua shaba. Hiramu alikuwa na hekima nyingi na akili, na fundi stadi wa kazi yoyote ya shaba. Basi, alikuja kwa mfalme Solomoni, akamfanyia kazi yake yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa shina la Nafutali, naye baba yake alikuwa mtu wa Tiro aliyefua shaba. Huyu alikuwa mwenye werevu wa kweli na utambuzi na ujuzi wote wa kuzitengeneza kazi zote pia kwa shaba. Huyu akaja kwa mfalme Salomo, akamfanyizia hizo kazi zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila ya Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, mstadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikilia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo alikuwa mwana wa mujane wa kabila la Nafutali, na baba yake alikuwa mukaaji wa Tiro, mufua-shaba. Hiramu alikuwa na hekima nyingi na akili, fundi kabisa wa kazi yoyote ya shaba. Basi, alikuja kwa mufalme Solomono, akamufanyia kazi yake yote.