1 Kings 7:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, akajenga jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 44.5, upana wake mita 22.25, na kimo chake mita 13.5. Ilikuwa imejengwa juu ya safu 3 za nguzo za mierezi, nguzo ambazo zilishikilia boriti za mierezi kwa upande wa juu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alijenga jumba lililoitwa Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. Lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, upana wa dhiraa hamsini, na kimo cha dhiraa thelathini, na safu nne za nguzo za mwerezi zilizoshikilia boriti za mwerezi zilizosawazishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa aliijenga nyumba ya mwitu wa Lebanoni; mikono mia urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, akajenga jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 44.5, upana wake mita 22.25, na kimo chake mita 13.5. Ilikuwa imejengwa juu ya safu 3 za nguzo za mierezi, nguzo ambazo zilishikilia boriti za mierezi kwa upande wa juu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini, likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini, likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha alijenga nyumba ya msitu wa Lebanoni; mikono mia moja urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, akajenga jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 44.5, upana wake mita 22.25, na kimo chake mita 13.5. Ilikuwa imejengwa juu ya safu 3 za nguzo za mierezi, nguzo ambazo zilishikilia boriti za mierezi kwa upande wa juu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwanza akaijenga nyumba ya mwituni kwa Libanoni, urefu wake wa kwenda mbele ulikuwa mikono mia nao upana wake mikono hamsini nao urefu wake wa kwenda juu mikono thelathini; ilikuwa juu ya safu nne za nguzo za miangati, nazo boriti za miangati zilikuwa zimewekwa juu ya hizo nguzo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa aliijenga nyumba ya mwitu wa Lebanoni; mikono mia urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, akajenga jengo lililoitwa Nyumba ya pori ya Lebanoni. Urefu wake ulikuwa metre makumi ine na ine na nusu, upana wake metre makumi mbili na mbili na sentimetre makumi mbili na tano, na urefu wake wa kwenda juu metre kumi na tatu na nusu. Ilikuwa imejengwa juu ya mistari mitatu ya nguzo za mierezi, nguzo ambazo zilishikilia boriti za mierezi kwa upande wa juu.