1 Kings 7:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Taji hizo zilikuwa juu ya hizo nguzo mbili, na pia zilikuwa juu ya sehemu ya mviringo iliyojitokeza karibu na zile nyavu. Palikuwa na mifano 400 ya matunda ya mkomamanga, imepangwa safu mbili kuzunguka kila taji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Juu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga mia mbili katika safu kuzunguka pande zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji ya pili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Taji hizo zilikuwa juu ya hizo nguzo mbili, na pia zilikuwa juu ya sehemu ya mviringo iliyojitokeza karibu na zile nyavu. Palikuwa na mifano 400 ya matunda ya mkomamanga, imepangwa safu mbili kuzunguka kila taji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Juu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga 200 katika safu kuzunguka pande zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Juu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga 200 katika safu kuzunguka pande zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji la pili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Taji hizo zilikuwa juu ya hizo nguzo mbili, na pia zilikuwa juu ya sehemu ya mviringo iliyojitokeza karibu na zile nyavu. Palikuwa na mifano 400 ya matunda ya mkomamanga, imepangwa safu mbili kuzunguka kila taji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo vichwa vya juu ya hizo nguzo vilikuwa juu penye ukingo uliokuwa wenye ile misuko. Nazo komamanga zilikuwa 200, zikauzunguka nao msuko wa nguzo ya pili kwa mistari-mistari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji ya pili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Taji hizo zilikuwa juu ya hizo nguzo mbili, na vilevile zilikuwa juu ya sehemu ya muviringo iliyojitokeza karibu na zile nyavu. Kulikuwa mifano mia ine ya matunda ya makomamanga, imepangwa kwa mistari miwili kuzunguka kila taji.