1 Kings 7:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hiramu aliziweka nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu; nguzo aliyoisimika upande wa kusini iliitwa Yakini, na ile aliyoisimika upande wa kaskazini iliitwa Boazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hiramu akazisimamisha zile nguzo barazani pa Hekalu. Nguzo iliyokuwa upande wa kusini akaiita Yakini, na ile ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kuume, akaiita jina lake Yakini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hiramu aliziweka nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu; nguzo aliyoisimika upande wa kusini iliitwa Yakini, na ile aliyoisimika upande wa kaskazini iliitwa Boazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hiramu akasimamisha nguzo kwenye baraza ya Hekalu. Nguzo ya upande wa kusini akaiita Yakini na ile ya upande wa kaskazini Boazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hiramu akasimamisha nguzo kwenye baraza ya Hekalu. Nguzo ya upande wa kusini akaiita Yakini, na ile ya upande wa kaskazini Boazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kulia, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto, akaiita jina lake Boazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hiramu aliziweka nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu; nguzo aliyoisimika upande wa kusini iliitwa Yakini, na ile aliyoisimika upande wa kaskazini iliitwa Boazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akazisimamisha hizo nguzo penye ukumbi wa jumba hili; alipoisimamisha nguzo ya kuumeni akaiita jina lake Yakini (Hushikiza); tena alipoisimamisha nguzo ya kushotoni akaiita jina lake Boazi (Nguvu imo).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kuume, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto, akaiita jina lake Boazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiramu aliziweka nguzo hizo kwenye baraza ya hekalu; nguzo aliyoisimika upande wa kusini iliitwa Yakini, na ile aliyoisimika upande wa kaskazini iliitwa Boazi.