1 Kings 7:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hiramu alitengeneza Birika liitwalo Bahari. Lilikuwa la mviringo lenye upana wa mita 4.5 kutoka ukingo hadi ukingo, na urefu wa mita 2.25 na mzingo wa mita 13.5.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hiramu akasubu Bahari ya chuma, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo, na kimo cha dhiraa tano. Mzunguko wake ulikuwa dhiraa thelathini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hiramu alitengeneza Birika liitwalo Bahari. Lilikuwa la mviringo lenye upana wa mita 4.5 kutoka ukingo hadi ukingo, na urefu wa mita 2.25 na mzingo wa mita 13.5.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hiramu akasubu Bahari ya chuma, yenye umbo la mviringo, vipimo vyake dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Mzunguko wake ulikuwa dhiraa thelathini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hiramu akasubu Bahari ya chuma, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Mzunguko wake ulikuwa dhiraa thelathini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena akatengeneza bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hiramu alitengeneza Birika liitwalo Bahari. Lilikuwa la mviringo lenye upana wa mita 4.5 kutoka ukingo hadi ukingo, na urefu wa mita 2.25 na mzingo wa mita 13.5.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaitengeneza ile bahari kwa shaba iliyoyeyushwa; toka ukingo wake wa huku hata ukingo wa huko ilikuwa mikono kumi; iliviringana pande zote, urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mikono mitano, nayo kamba ya kuizunguka pande zote ilikuwa ya mikono thelathini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiramu alitengeneza birika la maji la muviringo lenye upana wa metre ine na nusu kutoka ukingo mpaka ukingo, na urefu wa metre mbili na sentimetre makumi mbili na muzunguko wa metre kumi na tatu na nusu.