1 Kings 7:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chini ya ukingo wake, kulizunguka tangi hilo, kulikuwa na safu mbili za vibuyu, kila kimoja mita 13.5. Vibuyu hivyo vilikuwa vimetengenezwa wakati huohuo tangi hilo lilipofanywa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Chini ya ukingo, ilizungukwa na mapambo ya maboga kumi kwa kila dhiraa. Maboga hayo yalikuwa yamesubiwa katika safu mbili ili kuwa kitu kimoja na hiyo Bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na chini ya ukingo wake kulikuwa na maboga yaliyoizunguka, kwa mikono kumi, yakiizunguka bahari; kulikuwa na safu mbili za hayo maboga, yakafanywa kalibuni hapo bahari ilipofanywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chini ya ukingo wake, kulizunguka tangi hilo, kulikuwa na safu mbili za vibuyu, kila kimoja mita 13.5. Vibuyu hivyo vilikuwa vimetengenezwa wakati huohuo tangi hilo lilipofanywa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Chini ya ukingo, ilizungukwa na maboga, kumi kwenye kila dhiraa moja. Maboga yalikuwa yamesubiwa katika safu mbili ili kuwa kitu kimoja na hiyo bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Chini ya ukingo, ilizungukwa na maboga, kumi kwenye kila dhiraa moja. Maboga yalikuwa yamesubiwa katika safu mbili ili kuwa kitu kimoja na hiyo bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na chini ya ukingo wake kulikuwa na maboga yaliyoizunguka, kwa mikono kumi, yakiizunguka bahari; kulikuwa na safu mbili za hayo maboga, yakafanywa katika kalibu hapo bahari ilipofanywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chini ya ukingo wake, kulizunguka tangi hilo, kulikuwa na safu mbili za vibuyu, kila kimoja mita 13.5. Vibuyu hivyo vilikuwa vimetengenezwa wakati huohuo tangi hilo lilipofanywa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Chini ya ukingo wake kuizunguka pande zote palikuwa na mifano ya matango, kumi kwa mkono mmoja, ikaizunguka hiyo bahari pande zote, hiyo mifano ya matango ilikuwa mistari miwili, nayo ilikuwa imeyeyushiwa mumo, bahari ilipoyeyushwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na chini ya ukingo wake kulikuwa na maboga yaliyoizunguka, kwa mikono kumi, yakiizunguka bahari; kulikuwa na safu mbili za hayo maboga, yakafanywa kalibuni hapo bahari ilipofanywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chini ya ukingo wake, kulizunguka birika hilo, kulikuwa mistari miwili ya vibuyu, kila kimoja metre kumi na tatu na nusu. Vibuyu hivyo vilikuwa vimetengenezwa wakati uleule birika lile lilipofanywa.