1 Kings 7:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nalo tangi lilikuwa limewekwa juu ya sanamu za mafahali kumi na wawili; tatu zikielekea upande wa kaskazini, tatu zikielekea magharibi, tatu kusini, na nyingine tatu mashariki. Tangi liliwekwa juu ya mafahali hao, sehemu zao za nyuma zikiwa ndani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ile Bahari iliwekwa juu ya mafahali kumi na wawili, watatu wakielekea kaskazini, watatu wakielekea magharibi, watatu wakielekea kusini, na watatu wakielekea mashariki. Hiyo Bahari iliwekwa juu yao, na sehemu zao za nyuma zilielekeana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nalo tangi lilikuwa limewekwa juu ya sanamu za mafahali kumi na wawili; tatu zikielekea upande wa kaskazini, tatu zikielekea magharibi, tatu kusini, na nyingine tatu mashariki. Tangi liliwekwa juu ya mafahali hao, sehemu zao za nyuma zikiwa ndani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bahari iliwekwa juu ya mafahali kumi na wawili, watatu wakielekea kaskazini, watatu wakielekea magharibi, watatu wakielekea kusini na watatu wakielekea mashariki. Bahari iliwekwa juu yao na sehemu zao za nyuma zilielekeana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bahari iliwekwa juu ya mafahali kumi na wawili, watatu wakielekea kaskazini, watatu wakielekea magharibi, watatu wakielekea kusini na watatu wakielekea mashariki. Bahari iliwekwa juu yao na sehemu zao za nyuma zilielekeana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nalo tangi lilikuwa limewekwa juu ya sanamu za mafahali kumi na wawili; tatu zikielekea upande wa kaskazini, tatu zikielekea magharibi, tatu kusini, na nyingine tatu mashariki. Tangi liliwekwa juu ya mafahali hao, sehemu zao za nyuma zikiwa ndani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na mbili, tatu zilielekea kaskazini, tatu zilielekea baharini, tatu zilielekea kusini, tatu zilielekea maawioni kwa jua, nayo bahari ilikuwa juu yao, nayo mapaja yao yote yalikuwa yameelekea ndani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikakaa juu ya ng’ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nalo birika lilikuwa limewekwa juu ya sanamu za ngombe dume kumi na wawili; tatu zikielekea upande wa kaskazini, tatu zikielekea upande wa magaribi, tatu kusini, na nyingine tatu mashariki. Birika liliwekwa juu ya ngombe dume hao, sehemu zao za nyuma zikiwa ndani.