1 Kings 7:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimita 7.5; nao ulikuwa ukifanana na ukingo wa kikombe na kama ua la yungiyungi. Tangi liliweza kujaa maji kiasi cha lita 40,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bahari hiyo ilikuwa na unene wa nyanda moja, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi lililochanua; nayo ingejazwa na bathi elfu mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimita 7.5; nao ulikuwa ukifanana na ukingo wa kikombe na kama ua la yungiyungi. Tangi liliweza kujaa maji kiasi cha lita 40,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa na unene wa nyanda nne na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 2,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa na unene wa nyanda nne na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 2,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimita 7.5; nao ulikuwa ukifanana na ukingo wa kikombe na kama ua la yungiyungi. Tangi liliweza kujaa maji kiasi cha lita 40,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unene wake ulikuwa upana wa shibiri, nao ukingo wake wa juu ulikuwa kama wa kikombe au kama wa ua la uwago. Ndani yake zilienea bati 2000, ndip pishi 18000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimetre saba na nusu; nao ulikuwa ukifanana na ukingo wa kikombe na kama ua la yungiyungi. Birika liliweza kujaa maji kadiri ya litre elfu makumi ine.