1 Kings 7:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Isitoshe, kila gari lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyazungukia magurudumu hayo, vilikuwa vya shaba. Kwenye pembe nne za gari kulikuwa na vishikizo vya shaba kwa ajili ya birika kubwa. Karibu ya kila kishikio kuliwekwa mapambo ya maua ya kusokotwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya kuyazungusha. Kila kitako kilikuwa na sinia iliyowekwa juu ya vishikizo vinne viliyosubiwa shada za maua kila upande.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila tako lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Isitoshe, kila gari lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyazungukia magurudumu hayo, vilikuwa vya shaba. Kwenye pembe nne za gari kulikuwa na vishikizo vya shaba kwa ajili ya birika kubwa. Karibu ya kila kishikio kuliwekwa mapambo ya maua ya kusokotwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyazungusha hayo magurudumu na kila kimoja kilikuwa na sinia kwenye vishikizo vinne vya taji iliyosubiwa kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyazungusha hayo magurudumu na kila kimoja kilikuwa na sinia kwenye vishikizo vinne vya taji iliyosubiwa kila upande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Isitoshe, kila gari lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyazungukia magurudumu hayo, vilikuwa vya shaba. Kwenye pembe nne za gari kulikuwa na vishikizo vya shaba kwa ajili ya birika kubwa. Karibu ya kila kishikio kuliwekwa mapambo ya maua ya kusokotwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila kilingo kimoja kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, navyo vyuma vya kuyashikia vilikuwa vya shaba; tena miguu yao minne ilikuwa yenye vishikio, navyo hivi vishikio vilikuwa vimetiwa kwa kuyeyushwa chini ya bakuli, tena kando yao kila mmoja pametiwa kata zilizoelekeana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila tako lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila gari lilikuwa na magurudumu mane ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyashika magurudumu hayo, vilikuwa vya shaba. Kwenye pembe ine za gari kulikuwa vikingio vya shaba kwa ajili ya birika kubwa. Karibu ya kila kikingio kuliwekwa mapambo ya maua ya kusokotwa.