1 Kings 7:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na hayo magurudumu manne yalikuwa chini ya yale mabamba; vyuma vya katikati kuzunguka magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa na mfumo wa gari lenyewe; na kimo cha magurudumu hayo kilikuwa sentimita 66.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yale magurudumu manne yalikuwa chini ya papi, na vyuma vya kuyazungushia viliunganishwa kwenye kitako. Kipenyo cha kila gurudumu kilikuwa dhiraa moja na nusu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na magurudumu manne yalikuwa chini ya papi; na mikono ya magurudumu ndani ya tako; na kwenda juu kwake gurudumu moja mkono mmoja na nusu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na hayo magurudumu manne yalikuwa chini ya yale mabamba; vyuma vya katikati kuzunguka magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa na mfumo wa gari lenyewe; na kimo cha magurudumu hayo kilikuwa sentimita 66.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Magurudumu manne yalikuwa chini ya papi, na vyuma vya katikati vya kuzungushia magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa kwenye kitako. Kipenyo cha kila gurudumu kilikuwa dhiraa moja na nusu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Magurudumu manne yalikuwa chini ya papi, na vyuma vya katikati vya kuzungushia magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa kwenye kitako. Kipenyo cha kila gurudumu kilikuwa dhiraa moja na nusu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na magurudumu manne yalikuwa chini ya papi; na mikono ya magurudumu ndani ya vitako; na kwenda juu kwake gurudumu moja mkono mmoja na nusu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na hayo magurudumu manne yalikuwa chini ya yale mabamba; vyuma vya katikati kuzunguka magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa na mfumo wa gari lenyewe; na kimo cha magurudumu hayo kilikuwa sentimita 66.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yale magurudumu manne yalikuwa chini ya vibao vya kufungia, navyo vyuma vya kuyashikia magurudumu vilikuwa vimeungwa na kilingo, nao urefu wa kwenda juu wa gurudumu moja ulikuwa mkono mmoja na nusu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na magurudumu manne yalikuwa chini ya papi; na mikono ya magurudumu ndani ya tako; na kwenda juu kwake gurudumu moja mkono mmoja na nusu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na hayo magurudumu mane yalikuwa chini ya vile vibandiko; vyuma vya katikati kwa kushika magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa na majengo ya gari lenyewe; na urefu wa kwenda juu wa magurudumu hayo ulikuwa sentimetre makumi saba na tano.