1 Kings 7:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwenye nafasi wazi iliyopatikana katika vishikio na mabamba ya kila gari, Hiramu alichonga michoro ya viumbe wenye mabawa, simba na miti ya mitende, akazungushia na mashada ya mapambo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliweka nakshi za makerubi, simba na mitende juu ya vishikio na juu ya papi, katika kila nafasi, na shada za maua kuzunguka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akachora juu ya mabamba ya mashikio yake, na juu ya papi zake, makerubi, na simba, na mitende, moja moja kama ilivyokuwa nafasi, na masongo pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwenye nafasi wazi iliyopatikana katika vishikio na mabamba ya kila gari, Hiramu alichonga michoro ya viumbe wenye mabawa, simba na miti ya mitende, akazungushia na mashada ya mapambo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alitia nakshi za makerubi, simba na miti ya mitende juu ya uso wa vishikio na juu ya papi, katika kila nafasi iliyopatikana, pamoja na mataji yaliyosokotwa kuzunguka pande zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alitia nakshi za makerubi, simba na miti ya mitende juu ya uso wa vishikio na juu ya papi, katika kila nafasi iliyopatikana, pamoja na mataji yaliyosokotwa kuzunguka pande zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akachora juu ya mabamba ya mashikio yake, na juu ya papi zake, makerubi, na simba, na mitende, moja moja kama ilivyokuwa nafasi, na masongo pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwenye nafasi wazi iliyopatikana katika vishikio na mabamba ya kila gari, Hiramu alichonga michoro ya viumbe wenye mabawa, simba na miti ya mitende, akazungushia na mashada ya mapambo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mabamba ya vyuma vyake vya kushikia na katika vibao vyake vya kufungia akachora Makerubi na simba na mitende, po pote kama palivyokuwa na nafasi, kisha akachora kata za maua za kuyazungusha yale machoro.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akachora juu ya mabamba ya mashikio yake, na juu ya papi zake, makerubi, na simba, na mitende, moja moja kama ilivyokuwa nafasi, na masongo pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenye nafasi wazi iliyopatikana katika vikingio na vibandiko vya kila gari, Hiramu alichonga michoro ya makerubi, simba na miti ya ngazi, akazungusha mashada ya mapambo.