1 Kings 7:48 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alitengeneza vifaa vyote vilivyokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu: Madhabahu ya dhahabu, meza ya dhahabu kwa ajili ya mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu: madhabahu ya dhahabu; meza ya dhahabu za kuweka mikate ya Wonesho;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Bwana; madhabahu ya dhahabu, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya dhahabu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alitengeneza vifaa vyote vilivyokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu: madhabahu ya dhahabu, meza ya dhahabu kwa ajili ya mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Solomoni akatengeneza samani zote kwa ajili ya Hekalu la BWANA: madhabahu ya dhahabu; meza ya dhahabu ambayo juu yake ndipo palipokuwa mikate Mitakatifu;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la bwana: madhabahu ya dhahabu; meza ya dhahabu za kuweka mikate ya Wonyesho;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akavitengeneza vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa BWANA; madhabahu ya dhahabu, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya dhahabu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alitengeneza vifaa vyote vilivyokuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu: Madhabahu ya dhahabu, meza ya dhahabu kwa ajili ya mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Salomo alivyovitengeneza vyombo vyote vya kutumiwa nyumbani mwa Bwana. Lakini meza ya kutambikia ilikuwa ya dhahabu, nayo meza ya kumwekea Bwana mikate ilikuwa ya dhahabu;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa BWANA; madhabahu ya dhahabu, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya dhahabu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alitengeneza vifaa vyote vilivyokuwa katika nyumba ya Yawe: mazabahu ya zahabu meza kwa ajili ya mikate ya kuwekwa mbele ya Mungu –meza ile ilifunikwa na zahabu– vinara vya taa vilivyowekwa mbele ya Pahali Patakatifu Sana, vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini –vilifunikwa na zahabu safi– maua taa koleo –vilifunikwa na zahabu– vikombe makasi ya kukata tambi za mishumaa mabakuli vyetezo vya kuwekea ubani miko ya kuopoa moto –vilifunikwa na zahabu safi– vyuma vya kushika milango ya sehemu ya Pahali Patakatifu Sana vyuma vya kushika milango ya hekalu –vilifunikwa na zahabu.