1 Kings 8:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mfalme Sulemani akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la Bwana kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mfalme Solomoni akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la BWANA kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Mfalme Sulemani akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa makabila na wakuu wa koo za wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mfalme Solomoni akawakutanisha mbele yake huko Yerusalemu wazee na viongozi wote wa makabila na wa koo za Israeli ili waliondoe sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu katika mji wa Daudi, yaani Siyoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Salomo akawakusanya wazee wa Waisiraeli nao wote waliokuwa vichwa vya mashina na wakuu wa milango ya wana wa Isiraeli mle Yerusalemu kwake yeye mfalme Salomo kwenda kulitoa Sanduku la Agano la Bwana katika mji wa Dawidi ulioitwa Sioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme Solomono akawakusanya mbele yake kule Yerusalema wazee na viongozi wote wa makabila na wa ukoo za Waisraeli kusudi waliondoe Sanduku la Agano la Yawe katika muji wa Daudi, ni kusema Sayuni.