1 Kings 8:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
‘Tangu niwaondoe watu wangu Israeli nchini Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; ila nilimchagua Daudi, atawale watu wangu, Israeli.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo na Jina langu liwe humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wo wote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nalimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
‘Tangu niwaondoe watu wangu Israeli nchini Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; ila nilimchagua Daudi, atawale watu wangu, Israeli.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lo lote la Israeli Hekalu lijengwe kwa ajili ya Jina langu ili lipate kuwako huko, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wowote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nilimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
‘Tangu niwaondoe watu wangu Israeli nchini Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; ila nilimchagua Daudi, atawale watu wangu, Israeli.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tangu siku ile, nilipoutoa ukoo wangu wa Waisiraeli huko Misri, sikuchagua mji katika mashina yote ya Isiraeli, ndimo wanijengee Nyumba, Jina langu likae humo. Lakini nilimchagua Dawidi wa kuutawala ukoo wangu wa Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wo wote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nalimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
‘Tangu nilipowaondoa watu wangu Waisraeli katika inchi ya Misri, sikuchagua muji wowote katika makabila ya Waisraeli kusudi nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; lakini nilimuchagua Daudi, atawale watu wangu, Waisraeli.’