1 Kings 8:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ichunge nyumba hii usiku na mchana, mahali ambapo umesema, ‘Hapo ndipo watu watakapoliheshimu jina langu;’ unisikie ninapokuja mahali hapa kuomba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwa humo,’ ili upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ichunge nyumba hii usiku na mchana, mahali ambapo umesema, ‘Hapo ndipo watu watakapoliheshimu jina langu;’ unisikie ninapokuja mahali hapa kuomba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ichunge nyumba hii usiku na mchana, mahali ambapo umesema, ‘Hapo ndipo watu watakapoliheshimu jina langu;’ unisikie ninapokuja mahali hapa kuomba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uwe macho kuiangalia Nyumba hii usiku na mchana, ipate kuwa mahali pale, ulipopasema: Mahali hapa ndipo, Jina langu litakapokuwa! Kwa hiyo yasikie maombo, mtumishi wako atakayokuomba mahali hapa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uchunge nyumba hii usiku na muchana, nafasi ambapo umesema: ‘Hapo ndipo watu watakapoliheshimu jina langu’. Unisikilize ninapokuja pahali hapa kwa kuomba.