1 Kings 8:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikia maombi yangu mimi mtumishi wako na ya watu wako Israeli wanapoomba wakielekea mahali hapa. Usikie maombi kutoka huko mbinguni; na ukisha sikia, utusamehe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia ukiwa mbinguni, makao yako, na unaposikia, samehe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikia maombi yangu mimi mtumishi wako na ya watu wako Israeli wanapoomba wakielekea mahali hapa. Usikie maombi kutoka huko mbinguni; na ukisha sikia, utusamehe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikia maombi yangu mimi mtumishi wako na ya watu wako Israeli wanapoomba wakielekea mahali hapa. Usikie maombi kutoka huko mbinguni; na ukisha sikia, utusamehe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yasikie nayo malalamiko ya mtumishi wako nayo yao walio ukoo wako wa Waisiraeli, watakayokuomba mahali hapa! Wewe wasikie huko juu mbinguni, unakokaa! Tena utakapowasikia uwaondolee makosa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uisikie dua ya mtumwa wako, na ya watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, sikia huko mbinguni, makao yako; nawe usikiapo, samehe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usikilize wakati tunapokusihi, mimi mutumishi wako na watu wako Waisraeli ambao tutaomba tukielekea pahali hapa. Kutokea kwako mbinguni, usikilize. Na ukisha kusikiliza, utusamehe.