1 Kings 8:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ikiwa watu wako Waisraeli, wameshindwa na adui zao kwa sababu ya dhambi walizotenda dhidi yako, nao wakitubu kwako na kulikiri jina lako, wakiomba msamaha wako kwa unyenyekevu katika nyumba hii,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, nao wakakugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ikiwa watu wako Waisraeli, wameshindwa na adui zao kwa sababu ya dhambi walizotenda dhidi yako, nao wakitubu kwako na kulikiri jina lako, wakiomba msamaha wako kwa unyenyekevu katika nyumba hii,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ikiwa watu wako Waisraeli, wameshindwa na adui zao kwa sababu ya dhambi walizotenda dhidi yako, nao wakitubu kwako na kulikiri jina lako, wakiomba msamaha wako kwa unyenyekevu katika nyumba hii,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, walio ukoo wako wa Waisiraeli wakimbizwe na adui, kwa kuwa wamekukosea; kisha watakapokurudia na kuliungama Jina lako, wakuombe na kukulalamikia humu Nyumbani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea tena kwako, na kulikiri jina lako wakikuomba na kukusihi katika nyumba hii;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ikiwa watu wako Waisraeli wameshindwa na waadui zao kwa sababu ya zambi walizotenda mbele yako, nao wakikugeukia na kusifu jina lako, wakiomba na kukusihi katika nyumba hii,