1 Kings 8:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tafadhali, uwasikie kutoka huko mbinguni, na usamehe dhambi za watumishi wako, watu wako Israeli, huku ukiwafundisha kufuata njia nyofu; ukanyeshe mvua katika nchi yako hii ambayo uliwapa watu wako iwe mali yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
basi usikie ukiwa mbinguni, usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi, na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tafadhali, uwasikie kutoka huko mbinguni, na usamehe dhambi za watumishi wako, watu wako Israeli, huku ukiwafundisha kufuata njia nyofu; ukanyeshe mvua katika nchi yako hii ambayo uliwapa watu wako iwe mali yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua katika nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tafadhali, uwasikie kutoka huko mbinguni, na usamehe dhambi za watumishi wako, watu wako Israeli, huku ukiwafundisha kufuata njia nyofu; ukanyeshe mvua katika nchi yako hii ambayo uliwapa watu wako iwe mali yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wewe na uwasikie huko mbinguni, uwaondolee makosa yao walio watumishi wako nayo yao walio ukoo wako wa Waisiraeli! Kisha wafundishe njia iliyo njema, waishike, upate kuinyeshea nchi yako mvua tena, kwa kuwa umeipa walio ukoo wako, iwe fungu lao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tafazali, uwasikilize kutokea kule mbinguni, usamehe zambi za watumishi wako, watu wako Waisraeli, na uwafundishe kufuata njia nzuri. Kisha unyeshe mvua katika inchi yako hii ambayo uliwapa watu wako kwamba itakuwa mali yao.