1 Kings 8:38 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
tafadhali, usikie maombi yoyote yatakayoombwa na watu wako, Israeli, au yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli; kila mtu akijua taabu za moyoni mwake, akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea kwenye nyumba hii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kila dua au ombi litakalotolewa na yeyote kati ya watu wako Israeli, akitambua taabu za moyo wake mwenyewe, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
tafadhali, usikie maombi yoyote yatakayoombwa na watu wako, Israeli, au yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli; kila mtu akijua taabu za moyoni mwake, akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea kwenye nyumba hii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akijua juu ya taabu ya moyo wake mwenyewe, akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu za moyo wake mwenyewe, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
maombi yoyote au dua yoyote ikifanywa na mtu yeyote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
tafadhali, usikie maombi yoyote yatakayoombwa na watu wako, Israeli, au yatakayoombwa na mtu yeyote au watu wako wote wa Israeli; kila mtu akijua taabu za moyoni mwake, akikuomba huku akinyosha mikono yake kuelekea kwenye nyumba hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, lisikie kila ombo na kila lalamiko litakalokutokea, kama ni la mtu mmoja awaye yote, au lao wote walio ukoo wako wa Waisiraeli, kwa kuwa kila mtu anayajua mapigo ya moyo wake. Hapo watakapokuja kuikunjua mikono yau humu Nyumbani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
maombi yo yote au dua yo yote ikifanywa na mtu awaye yote, au na watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu maradhi ya moyo wake, na kuikunjua mikono yake kuielekea nyumba hii;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
tafazali, chochote ambacho mutu yeyote au watu wako wote wa Waisraeli wanakuomba na kukusihi, kila mutu akijua taabu ndani ya moyo wake na kunyoosha mikono yake kuelekea nyumba hii,