1 Kings 8:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, usikie huko kwako mbinguni, utoe msamaha na kuchukua hatua; pia umtendee kila mtu kadiri anavyostahili (kwani ni wewe tu ujuaye mawazo ya mioyo ya wanadamu wote);
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
basi usikie ukiwa mbinguni, makao yako. Usamehe na utende; umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote),
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote);
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, usikie huko kwako mbinguni, utoe msamaha na kuchukua hatua; pia umtendee kila mtu kadiri anavyostahili (kwani ni wewe tu ujuaye mawazo ya mioyo ya wanadamu wote);
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote);
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, usikie huko kwako mbinguni, utoe msamaha na kuchukua hatua; pia umtendee kila mtu kadiri anavyostahili (kwani ni wewe tu ujuaye mawazo ya mioyo ya wanadamu wote);
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wewe na uwasikie huko mbinguni kuliko na Kao lako la kukaa, uwaondolee makosa ukifanya yapasayo na kumrudishia kila mtu, kama njia zake zilivyo, kwa hivyo, unavyoujua moyo wake! Kwani wewe peke yako unaijua mioyo ya wana wa watu wote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukasamehe, ukatende, ukampe kila mtu kwa kadiri ya njia zake; wewe ujuaye moyo wake; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu wote);
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, usikilize kule kwako mbinguni, uwasamehe na kumutendea kila mutu kwa kadiri anavyostahili, maana ni wewe tu unayejua mawazo ya mioyo ya wanadamu wote,