1 Kings 8:54 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Solomoni alipomaliza kusema sala hiyo yote na ombi lake kwa Mwenyezi-Mungu aliinuka kutoka pale mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiinua mikono yake juu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani alipomaliza dua na maombi haya yote kwa Mwenyezi Mungu, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiwa amenyoosha mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya Bwana, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Solomoni alipomaliza kusema sala hiyo yote na ombi lake kwa Mwenyezi-Mungu aliinuka kutoka pale mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiinua mikono yake juu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Solomoni alipomaliza dua hizi zote na maombi kwa BWANA, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya BWANA, mahali alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikawa imekunjuliwa kuelekea juu mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Sulemani alipomaliza dua hizi zote na maombi kwa bwana, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya bwana, mahali alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikawa imekunjuliwa kuelekea juu mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba BWANA maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya BWANA, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Solomoni alipomaliza kusema sala hiyo yote na ombi lake kwa Mwenyezi-Mungu aliinuka kutoka pale mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, mahali alipokuwa amepiga magoti akiinua mikono yake juu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo alipokwisha kumwomba Bwana maombo haya yote na kumlalamikia hivyo, akainuka hapo mbele ya meza ya kumtambikia Bwana, alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikiwa imekunjuliwa na kuelekea mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, Sulemani alipokwisha kumwomba BWANA maombi hayo, na dua hiyo yote, akasimama na kuondoka hapo mbele ya madhabahu ya BWANA, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua mikono yake kuelekea mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Solomono alipomaliza kusema maombi hayo yote na ombi lake kwa Yawe, alisimama kutoka pale mbele ya mazabahu ya Yawe, pahali alipokuwa amepiga magoti akiinua mikono yake juu.