1 Kings 8:63 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Solomoni alimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za amani: Ng'ombe 22,000 na kondoo 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote wa Israeli walivyoiweka wakfu nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani akatoa dhabihu sadaka za amani kwa Mwenyezi Mungu: ng’ombe elfu ishirini na mbili, pamoja na kondoo na mbuzi elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea Bwana, ng'ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Solomoni alimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za amani: ng'ombe 22,000 na kondoo 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote wa Israeli walivyoiweka wakfu nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akatoa dhabihu sadaka za amani kwa BWANA: ng'ombe 22,000, kondoo pamoja na mbuzi 120,000. Hivyo mfalme pamoja na Waisraeli wote wakaliweka wakfu Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akatoa dhabihu sadaka za amani kwa bwana: ng’ombe 22,000, pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea BWANA, ng'ombe elfu ishirini na mbili, na kondoo elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoiweka wakfu nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Solomoni alimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za amani: Ng'ombe 22,000 na kondoo 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na watu wote wa Israeli walivyoiweka wakfu nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akatoa ng'ombe 22000 na mbuzi na kondoo 120000 kuwa ng'ombe za tambiko za kumshukuru Bwana. Ndivyo, mfalme na wana wa Isiraeli wote walivyoieua Nyumba ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea BWANA, ng’ombe ishirini na mbili elfu, na kondoo mia na ishirini elfu. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoifanya wakfu nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Solomono alimutolea Yawe sadaka za amani: ngombe elfu makumi mbili na mbili na kondoo elfu mia moja na makumi mbili. Hivi ndivyo mufalme na watu wote wa Israeli walivyozindua nyumba ya Yawe.