1 Kings 8:64 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyohiyo, mfalme aliiweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwani hapo ndipo alipotolea sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba haikutosha sadaka hizo zote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hiyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Mwenyezi Mungu ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ile ile mfalme akaitakasa behewa ya katikati iliyokuwa mbele ya nyumba ya Bwana; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo, haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyohiyo, mfalme aliiweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwani hapo ndipo alipotolea sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba haikutosha sadaka hizo zote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku iyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya kati ya ua ulioko mbele ya Hekalu la BWANA na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za BWANA ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku iyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la bwana na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za bwana ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka ya amani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku ile ile mfalme akaitakasa behewa ya katikati iliyokuwa mbele ya nyumba ya BWANA; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za BWANA ilikuwa ndogo, haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyohiyo, mfalme aliiweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kwani hapo ndipo alipotolea sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba haikutosha sadaka hizo zote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo mfalme alikitakasa kipande cha kati cha ua uliokuwa mbele ya Nyumba ya Bwana, kwani ndiko, alikotolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vilaji vya tambiko na mafuta ya ng'ombe za tambiko za shukrani, kwani ile meza ya shaba ya kutambikia iliyokuwako kule mbele ya Bwana ilikuwa ndogo, haikueneza kabisa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vilaji vya tambiko na mafuta ya ng'ombe za tambiko za shukrani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ile ile mfalme akaitakasa behewa ya katikati iliyokuwa mbele ya nyumba ya BWANA; kwa kuwa hapo ndipo alipotoa sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na mafuta ya sadaka za amani; kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za BWANA ilikuwa ndogo, haikutosha kuzipokea sadaka za kuteketezwa, na sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyohiyo, mufalme aliizindua sehemu ya katikati ya uwanja uliokuwa mbele ya nyumba ya Yawe, maana ni pale ndipo alipotolea sadaka za kuteketezwa, sadaka za ngano, na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu ile mazabahu ya shaba haikutosha kwa sadaka hizo zote.