1 Kings 8:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapakuwa na kitu ndani ya sanduku la agano ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na Waisraeli walipotoka nchini Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndani ya Sanduku hapakuwa na kitu kingine isipokuwa vile vibao viwili vya mawe ambavyo Musa aliviweka ndani yake huko Horebu, mahali Mwenyezi Mungu alipofanya agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapakuwa na kitu ndani ya sanduku la agano ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na Waisraeli walipotoka nchini Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapakuwa na cho chote ndani ya Sanduku la Agano isipokuwa zile mbao mbili za mawe ambazo ziliwekwa na Mose huko Horebu, mahali ambapo BWANA alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili za mawe ambazo Musa alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapakuwa na kitu ndani ya sanduku la agano ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na Waisraeli walipotoka nchini Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mle Sandukuni hamkuwamo na kitu, ni zile mbao mbili za mawe tu, Mose alizoziweka humo huko Horebu, Bwana alipofanya Agano na wana wa Isiraeli, walipotoka katika nchi ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakukukuwa kitu ndani ya Sanduku la Agano lakini vile vibao viwili vya mawe ambavyo Musa aliviweka mule kule Horebu, pahali Yawe alipofanya agano na Waisraeli walipotoka katika inchi ya Misri.