1 Kings 9:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mfalme Solomoni alimpa Hiramu mfalme wa Tiro, miji ishirini katika mkoa wa Galilaya (kwa sababu huyo Hiramu alikuwa amempelekea Solomoni mbao za mierezi na miberoshi, na dhahabu pia, kadiri alivyohitaji kwa ujenzi).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Sulemani akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi na misunobari yote na dhahabu yote kama alivyohitaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mfalme Solomoni alimpa Hiramu mfalme wa Tiro, miji ishirini katika mkoa wa Galilaya (kwa sababu huyo Hiramu alikuwa amempelekea Solomoni mbao za mierezi na miberoshi, na dhahabu pia, kadiri alivyohitaji kwa ujenzi).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Solomoni akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Sulemani akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mfalme Solomoni alimpa Hiramu mfalme wa Tiro, miji ishirini katika mkoa wa Galilaya (kwa sababu huyo Hiramu alikuwa amempelekea Solomoni mbao za mierezi na miberoshi, na dhahabu pia, kadiri alivyohitaji kwa ujenzi).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, mfalme Salomo alipompa Hiramu, mfalme wa Tiro, miji ishirini katika nchi ya Galili, kwa kuwa alimpatia mfalme Salomo miti ya miangati na miti ya mivinje na dhahabu, yote pia, kama alivyoitaka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mufalme Solomono alimupa Hiramu mufalme wa Tiro miji makumi mbili katika jimbo la Galilaya kwa sababu yule Hiramu alikuwa amemupelekea Solomono mbao za mierezi na miberoshi, na zahabu vilevile, kadiri alivyohitaji kwa majengo.