1 Kings 9:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yafuatayo ni maelezo juu ya jinsi mfalme Solomoni alivyotumia kazi za kulazimishwa kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu, ikulu yake, ngome ya Milo na ukuta wa Yerusalemu, na pia katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Sulemani aliwafanyiza watu ili kulijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, na jumba lake la kifalme, na Milo, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, na Megido, na Gezeri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yafuatayo ni maelezo juu ya jinsi mfalme Solomoni alivyotumia kazi za kulazimishwa kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu, ikulu yake, ngome ya Milo na ukuta wa Yerusalemu, na pia katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ni maelezo kuhusu Mfalme Solomoni, jinsi alivyowafanyiza watu kazi za kulazimishwa ili kulijenga Hekalu la BWANA, jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe, Milo, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Sulemani, alivyowafanyiza watu ili kulijenga hekalu la bwana, na jumba lake la kifalme, na Milo, ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hasori, na Megido, na Gezeri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yafuatayo ni maelezo juu ya jinsi mfalme Solomoni alivyotumia kazi za kulazimishwa kujenga nyumba ya Mwenyezi-Mungu, ikulu yake, ngome ya Milo na ukuta wa Yerusalemu, na pia katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kazi za watu, mfalme Salomo aliowatoa kufanya kazi za nguvu, ni hizi: waliijenga Nyumba ya Bwana na nyumba yake na Milo na boma la kuuzunguka Yerusalemu, tena Hasori na Megido na Gezeri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, na Megido, na Gezeri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ni maelezo juu ya mufalme Solomono, jinsi alivyowatumikisha watu kazi za kulazimishwa katika kujenga nyumba ya Yawe, nyumba yake ya kifalme, uwanja wa Milo, na ukuta wa Yerusalema, na vilevile katika kujenga upya miji ya Hazori, Megido na Gezeri.