1 Kings 9:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Gezeri ndio mji ambao Farao, mfalme wa Misri, alikuwa ameuteka, akauchoma moto na kuwaua Wakanaani, wakazi wake. Baadaye, binti Farao alipoolewa na Solomoni, mfalme wa Misri alimpa binti yake mji huo wa Gezeri uwe zawadi ya harusi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Farao mfalme wa Misri alikuwa ameushambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Sulemani, kama zawadi ya arusi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
(Gezeri ndio mji ambao Farao, mfalme wa Misri, alikuwa ameuteka, akauchoma moto na kuwaua Wakanaani, wakazi wake. Baadaye, binti Farao alipoolewa na Solomoni, mfalme wa Misri alimpa binti yake mji huo wa Gezeri uwe zawadi ya harusi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Farao mfalme wa Misri alikuwa ameshambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Solomoni, kama zawadi ya arusi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Farao mfalme wa Misri alikuwa ameushambulia na kuuteka mji wa Gezeri. Alikuwa ameuchoma moto. Akawaua Wakanaani waliokuwa wakikaa humo na kisha kuutoa kwa binti yake, yaani mkewe Sulemani, kama zawadi ya arusi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
(Gezeri ndio mji ambao Farao, mfalme wa Misri, alikuwa ameuteka, akauchoma moto na kuwaua Wakanaani, wakazi wake. Baadaye, binti Farao alipoolewa na Solomoni, mfalme wa Misri alimpa binti yake mji huo wa Gezeri uwe zawadi ya harusi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda, akauteka Gezeri, akauteketeza kwa moto, nao Wakanaani waliokaa humo, akawaua, kisha akampa mwanawe aliyekuwa mkewe Salomo, uwe tunzo lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gezeri ndio muji ambao mufalme wa Misri alikuwa ameuteka, akauchoma kwa moto na kuwaua Wakanana, wakaaji wake. Nyuma, binti wa mufalme wa Misri alipoolewa na Solomono, mufalme wa Misri alimupa binti yake muji ule wa Gezeri ukuwe zawadi ya arusi.